Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Aayatullah Husayn Nūrī Hamadānī, mmoja wa marāji‘ adhim, katika mnasaba wa kufanyika kumbukumbu ya kuheshimu na kuenzi sura zilizobakia katika medani ya utukuzaji wa Ahlul-Bayt (‘alayhimus-salām), iliyofanyika katika Markaz ya Fiqhī A’immat al-Aṭhār (‘alayhimus-salām) katika mji wa Qom nchini Iran, alitoa ujumbe ambao matni yake kamili ni kama ifuatavyo:
بسم الله الرحمن الرحیم الحمد لله ربّ العالمین و الصلاة و السلام علی سیدنا و نبینا أبی القاسم المصطفی محمد و علی أهل بیته الطیبین الطاهرین، سیما بقیةالله فی الأرضین.
سلام علیکم و رحمةالله و برکاته
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia fursa ya kushiriki katika kikao hiki ambacho ni kwa ajili ya kuwaenzi watumishi wa Ahlul-Bayt (‘alayhimus-salām).
Bila shaka, kuwatumikia Maasumiin (‘alayhimus-salām), hasa kwa Hadhrat Sayyidush-Shuhadaa (‘alayhis-salām), ni hadhi na nafasi ya juu na bora kabisa katika ulimwengu huu; nafasi ambayo kama ikiambatana na ikhlāṣ, basi haina mfano wake.
Watu wote wakubwa katika historia walitamani majina yao yaandikwe katika orodha hii tukufu, na vitabu vyetu vya riwāyah vimejaa riwāyah ambazo zinatia nuru nyoyo zetu kuhusu jambo hili, kiasi kwamba haiwezekani kufafanuliwa kwa mapana hapa.
Lakini kwa ajili ya kupata baraka, nitataja riwāyah moja:
Abū ‘Amārah, mshairi, alifika kwa Imām Ṣādiq (‘alayhis-salām), Im'am akamwambia: “Ewe Abū Amārah! Nisomee mashairi kuhusu Imām Husayn (‘alayhis-salām).”
Anasema: Nikaanza kusoma mashairi. Imām akawa analia, kiasi cha kwamba sauti ya kilio chake ikawa inasikika mbali.
Kisha akasema: “Ewe Abū ‘Amārah! Yeyote atakayesoma shairi kuhusu Imām Husein (alayhis-salām) na akawafanya waty hamsini au thelathini au ishirini au wawili au hata mmoja kulia, malipo yake yatakuwa ni Pepo.”
Naam, umuhimu wa jambo hili uko juu kiasi hiki.
Hivyo basi, kuwaheshimu wasomaji Nauha na washairi waliomaliza maisha yao katika njia hii ni jambo la kuthaminiwa mno.
Kutoka nani nafsi yangu, namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anikubali mimi mja wake mnyonge kuwa ni miongoni mwa watumishi wa watukufu hawa, na kulikweka jina langu katika orodha hii tukufu.
Na leo ninakiri kuwa mimi ni mavumbi chini ya nyayo za watumishi wa Ahlul-Bayt (alayhimus-salām), hasa Hadhrat Sayyidush-Shuhadaa na Fāṭimah az-Zahrā (Salāmullāhi ‘alayhā).
Maoni yako